Wapi naweza kumpata Mungu?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Kwa usahihi kabisa mtu hawezi kumtafuta Mungu,lakini Mungu ndiye anayemtafuta na kumpata mwanadamu. Mungu anaishi mahali pa juu sana mahali ambapo mwanadamu hawezi kufika, lakini yeye amekuja na kufanya kuwa karibu na sisi na kututafuta. Mungu amejifunua peke yake katika sakramenti, neno lake (Biblia) katika ubatizo na ushirika mtakatifu pia katika maungamo ya dhambi na masamaha ya dhambi. Katika hayo inatupasa kumtafuta huko.

Kama umebatizwa inakupasa kujikumbusha mwenyewe hii ina maana gani. Katika ukiri wa imani ya mitume na kateksimo ni mahali pazuri pa kuanzia kujifunza hata kama hujabatizwa ni vizuri kuanzia hapo. Na pia nakutia moyo kusoma Biblia, anza kusoma agano jipya na zaidi INJILI.

Tafuta kanisa unaweza kupata ibada ya jumapili. Kipindi cha ibada unaweza pamoja na washirika kukiri na kuungama na kupokea tangazo la msamaha wa dhambi na kusikia mafundisho kutoka katika biblia. Kwa kupata ushirika mtakatifu tunakuwa karibu na Mungu. Mungu anakutana nasi katika mkate na katika mvinyo- mkate ukiwa ni mwili wa Kristo na mvinyo ukiwa ni damu ya Kristo.

“Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika nitawatia nguvu wagonjwa nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu nitawalisha hukumu."
(Ezekieli 34:16, SUV)

Bwana Mungu ninataka nikutafuta na kukujua wewe, nisaidie ni wapi nipate njia kwako