Ushiriki Mtakatifu ni Nini?

Mwandishi: 
Jari Rankinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Wakristo wanashiriki meza ya Bwana kama Yesu alivyoamuru. Wakati wote wanaposhiriki, maneno ya Yesu yanayofanya Ushirika mtakatifu yanasomwa. Yamechukuliwa kutoka katika maandiko matakatifu ya Biblia ambayo yanawaambia nini kilitokea Yerusalemu wakati wa usiku kabla ya kifo cha Bwana Yesu. Yesu na wanafunzi wake walisherehekea sakramenti, na Yesu aliwaambia kuendelea kufanya hivyo baadaye.

Katika maneno ya ushirika mtakatifu yanasema kwamba mkate ambao tunaumega ni mwili wa Bwana Yesu na Mvinyo ni agano jipya katika damu yake. Katika injili kutokana na Mathayo, Yesu alisema pia hii ni Damu yangu kwa hiyo mwili na Damu vipo pale katika ushirika mtakatifu.Ina maana kwamba Yesu yupo ndani ya mkate na katika mvinyo kwa njia maalum. Tunakutana naye na y eye anakutana na sisi. Wakati unafikiri wapi ningetakiwa kwenda kupata ukaribu na Yesu, nenda kwenye ushirika mtakatifu. Huu ni muujiza mkubwa wa ushirika mtakatifu. Yesu yuko pale na anafanya kazi nasi.

Katika ushirika mtakatifu mara nyingi unaweza kufikiri au kuhisi kwa uhakikakama kweli nitakutana na Yesu. Lakini mawazo yetu hayawezi kumzuia Yesu kuja karibu yetu. Yeye yupo palepale alipoahidi kuwa haijalishi ni kwa jinsi gani tunafikiri. Aliahidi kuwa kwenye ushirika mtakatifu-Mkate ni mwili wake, ana mvinyo ni damu yake.

"Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa Mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni mle; huu ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki, kwa maana hii ndio damu yangu ya agano, imwagikayokwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."
(Mathayo 26:26-28, SUV)