Nitaipataje Mbingu? Je nawezaje kuokoka?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Siku moja tajiri mmoja alimuuliza Yesu nitawezaje kuurithi uzima wa milele. Huyo tajiri alikuwa anaishi maisha mazuri. Yesu alimwambia auze mali zake zote na kuwapa maskini hizo fedha kisha amfuate Yesu. Tajiri alihuzunika sana. Wanafunzi walichanganyikiwa na kuanza kumuuliza Yesu maswali mengi. Ni vipi mtu anaweza kuokolewa­, Yesu aliwajibu, kwa wanadamu hilo haliwezekani bali kwa Mungu yote yanawezekana.

Ili ni jibu la Kikristo, tumefungwa kwa ubinafsiwetu wenyewe, tunajipenda wenyewe kuliko kuwapenda wenzetu. Nguvu zetu za kupata wokovu ni za Kibinafsi pia je Unalo tumaini lolote? Jibu la kikristo linatupa majibu ya tofauti na dini zingine mtazamo wetu si juu ya mwanadamu, na nini mwanadamu atafanya, mtazamo wetu ni juu ya Yesu Kristo. Yesu alifanya kile ambacho sisi tusingeweza kufanya. Alichukua mashtaka yetu mbele za Mungu na kupatanisha dhambi zetu na maovu yetu juu ya msalaba.

Pale umebaki ukamilifu wa msamaha wa dhambi ndani ya moyo wa Mungu uliyotangazwa kwetu kwa njia ya injili. Na tunapata hiyo kwa kupitia imani. Kupitia imani ndani ya Kristo tunaokolewa na kupata mbingu. Wakati nilipobatizwa katika jina la Mungu Baba na la mwana na la Roho mtakatifu natambua kwamba mimi ni mali ya Mungu sinta jaribu kuuliza kwa Mungu juu ya maisha yangu. Tunaweza kuwa na hakika kuhusu Yesu na kazi yake.

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu."
(Efeso 2:8-9, SUV)

Yesu nisaidie nikuamini wewe.