Mungu anasikia ombi langu?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Mungu anasikia maombi yote, lakini haina maana kwamba atajibu kwa wakati wote kama unavyoomba au kutarajia. Mungu si mashine ya kujibu maombi yote ambayo yapo k wake, lakini ni baba anayejua mahitaji ya watoto wake.

Anatupa kile ambacho ni kizuri kwa mwanga wa maisha ya milele. Kwa hiyo wakati mwingine anayajibu maombi yetu kwa kukataa matakwa yetu. Anatufanya sisi kusubiri na wakati mwingine anatupa majibu thabiti.

Kwa hilo tunaweza kuwa na uhakika kwamba wakati tunapoomba msamaha wa dhambi zetu kwa wokovu mara moja anaharakisha majibu. Tunaweza kusoma majibu yake kwa Biblia alipotoa ahadi ya kusamehe dhambi kwa wale wanaoungama dhambi zao.

“Au kuna mtu yupi kwenu ambaye mwanawe akimwomba atampa jiwe?Au akiomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu ,manajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?"
(Mathayo 7:9-11 SUV)

Mungu wakati mwingine nashangaa kama unanisikia ama la! Ahsante kwa kunisikia!