Imani inaanza lini?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Oscar Ulotu

Imani iokoayo siyo kazi ya mwanadamu bali ni zawadi itokayo kwa Mungu, itokayo nje ya mwanadamu. Mwanadamu hawezi kwa asili kuzalisha imani yeye mwenyewe au kuamua kuja katika imani, lakini mtu huwa na imani kupitia vyombo vya neema. Msingi wa kwanza wa vyombo vya neema ni neon la Mungu. Katika ubatizo imani inazalishwa kupitia neno lililochanganywa na maji. Na katika chakula cha Bwana imani iliyounganika na mkate na mvinyo na katika ungamo la dhambi inaunganishwa na msamaha wa dhambi.

Roho mtakatifu anazungumza na mtu kupitia neno la Mungu na kupitia neno hilo Roho mtakatifu anakuja ndani ya roho ya mwanadamu na kuzalisha imani, kuongeza na kuimarisha imani ni kazi muhimu za Roho Mtakatifu.

Kama unashangaa labda una imani au huna ya kutosha unaweza kumuomba Mungu akuimarishie imani, na ili niombe Mungu analojibu la usahihi unaweza kuamini kwamba Mungu anakupa imani au haijalishi ni aina gani unavyojihisi au unavyojizoesha.

Katika kanisa Roho anamtukuza Yesu Kristo kama mwokozi na kuhakikisha kwamba neema inakutosheleza pia. Imani siyo kitu chetu tunachokisukuma au kujaribu ila ni kazi ya Mungu ndani ya mtu.

"Basi imani, Chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."
(Rum 10:17, SUV)